5 Julai 2023 - 18:03
Kiongozi wa Ansarullah: Rukhsa kuvunjia heshima Qur'ani; lakini marukufu kufichua jinai za Wazayuni!

Kiongozi wa Harakati ya Ansarullah ya Yermen amekosoa kutoonyesha hisia ulimwengu wa Kiislamu kuhusiana na tukio la kuchomwa moto Qur'ani tukufu nchini Sweden na jinai za Wazayuni huko Palestina.

Badr al-Din al-Houthi amesema hayo katikka hotuba yake na kueleza kwamba, kufanyika mara kadhaa vitendo vya kuvunjiwa heshima Qur'ani tukufu katika nchi ya Sweden ni hatua zilizoratibiwa ambazo nyuma yake kuna lobi za Wazayuni.

Kiongozi huyo wa Ansarullah ameongeza kuwa, katika ulimwengu wa Magharibi vitendo vya kutusiwa na kuvunjiwa heshma Mitume na vitabu vya mbinguni vinaruhusiwa, lakini wakati huo huo ni marufuku kufichua jinai zinazofanywa na Wazayuni huko Palestina ni ithbati tosha kwamba, lobi za Kizayuni zina ushawishi mkubwa katika ulimwengu wa Magharibi.

Kuhusiana na radiamali ya ulimwengu wa Kiislamu kwa kitendo chga kuchomwa moto Qur'ani huko Sweden, kiongozi wa Ansarullah ya Yemen amesema, majibu ya kitendo hicho yanapaswa kuwa makubwa zaidi na yadhihirishe ghadhabu na hasira za Waislamu wote ulimwenguni.

Ameongeza kuwa, hatua ndogo kabisa inayioweza kuchukuuliiwa na ulimwengu wa Kiislamu kama jibu kwa kitendo hicho, ni kukata mataifa ya kiislamu uhusiano wa kidiplomasia na Sweden na kuisusia kiuchumi nchii hiyo.

Jumatano iliyopita ya tarehe 28 mwezi Juni raia mmoja wa Sweden alichoma moto na kuchana nakala ya Qur'ani Tukufu huko Stockholm. Kabla ya kuchoma moto Qur'ani Tukufu, Momika aliweka nyama ya nguruwe kwenye nakala ya kitabu hicho kitukufu, ambayo ni ishara ya kukidunisha na kukivunjia heshima kupitiliza kwa waumini wa dini ya Kiislamu. 

342/